Chanzo Halisi kutambulisha ‘Bila chanzo halisi hutoboi’ Aprili 28

Mtanzania
Published: Apr 15, 2024 07:22:00 EAT   |  Entertainment

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Msanii wa nyimbo za Injili ambaye aliwaikutamba kwenye Bongo Fleva na kundi la The Mafik Rhino ambaye kwa sasa ameokoka na anaitwa kwa jina la ‘Uelewa wa Sauti’ kuzindua albamu yao Aprili 28, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Akizungumza Aprili 14, 2024 na waandishi […]

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Msanii wa nyimbo za Injili ambaye aliwaikutamba kwenye Bongo Fleva na kundi la The Mafik Rhino ambaye kwa sasa ameokoka na anaitwa kwa jina la ‘Uelewa wa Sauti’ kuzindua albamu yao Aprili 28, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Aprili 14, 2024 na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Chanzo Halisi amesema kuwa jina la albamu hiyo ni ‘Bila Chanzo Halisi hutoboi’ amezumgumza na Wana Habari baada ya kumaliza zoezi la Usafi Tegeta.

Chanzo Halisi (Rhino) ameulizwa maswali iwapo ni kweli ameokoka au anafanya maigizo na kueleza kuwa kwa sasa anaishi maisha mengine na hakumbuki maisha ya nyuma aliyoishi wakati akifanya muziki za kizazi kipya.